Sunday, June 27, 2010

The opening of New Maisha Club

Usiku wa alhamisi palishika nguo kuchanika katika uzinduzi wa club mpya ya Maisha baada ya kukarabatiwa na kuongezwa ubora sasa imekuja kivingine huku ma DJ wa kimataifa wakipimana ubavu katika kuwarusha wapenzi wa burudani. Kabla ya kuungua karibu miezi 9 iliyopita Club Maisha ndio club iliyokuwa ikisumbua sana hapa jijini dar es salaam na kwa sasa imerudi upya na kwa mara ya kwanza tangu kutengenezwa upya.


Jana ilizinduliwa rasmi ikiwa na jina jipya la New Club Maisha huku wamiliki wa club hiyo wakiwadondosha ma DJ wakali kabisa hapa duniani mmoja akiwa ni mwanadada DJ L1 kutoka Las Vegas nchini Marekani ambae pia anashikilia taji la DJ bora wa kike duniani na mwingine akiwa na DJ Ape Man kutoka nchini Uganda ambaye ameweza kutesa vilivyo hata katika kumbi nyingi za starehe nchini uingereza.

Mwanadada huyo ambae jina lake halisi ni Lisa Mamalias anajulikana zaidi kwa jina la DJ L 1 anatesa sana katika club nyingi za marekani, leo atapiga nyimabo laivu ndani ya New Club Maishaa jijini Dar es salaam.
Akiongea na bongo5.com DJ huyo machachari alisema yupo hapa kwa ajili ya kuwarusha watanzania na ana imani kuwa watanzania watapata burudani ya kutosha kutoka kwake kwani yeye ana uzoefu wa kutosha kabisa.

“Nimekuja Tanzania kuwapa burudani na ninawaambia waje kwa wingi maana nameandaa burudani ya kutosha kabisa tegemeeni midundo mikali kabisa ya hip hop, top 40, reggae, na nyinginezo nyingi zinazotamba katika medani ya muziki duniani”.
…Akiendelea mwanadada huyo amesema ya kuwa yeye ni mzoefu wa kupiga kila aina ya muziki unaopendwa na kila mtu hivyo hakuna mtu atakae lala au kukaa kwenye kiti wakati yeye akiwa kwenye mashine.

“Ninapokuwa kwenye mashine hakuna mtu atakayelala kwa sababu naweza kupiga kila aina ya muziki hi vyo sidhani kama kuna mtu atakayeboreka wakati mimi nipo kwenye mashine” Kwa upande wa DJ Apeman yeye pia hakuwa kinyume na mwana dada huyo kwani amewaomba watanzania waje kushuhudia vitu adimu kutoka kwake “watanzania waje tu kwa wingi kwani nimewa andalia mipini ya kutosha kwa sababu ninaimani kuwa mambo nitakayoyafanya yatakuwa ni makubwa na pia hayajawahi kutokea Tanzania” Ma DJ hawa ambao ni wageni Tanzania walikuwa na mwnyeji wao ambaye ni DJ wa siku zote katika club hiyo ya Maisha anaejulikana kwa jina la DJ Zero.

No comments: